Tafakari ya Kitabu cha Kijivu
Je, tunataka kweli kuondokana na chuki zetu, hasira zetu, hofu zetu?
Gray Book, p. 46 (Step Six, Lines 20-21)
Maandishi Yetu ya Msingi yanatuambia kwamba kuna usalama fulani uliopotoka katika maumivu yanayojulikana. Wakati mwingine tunashikilia kasoro hizi kwa sababu wakati mmoja ndizo pekee tulizozijua. Kasoro hizi hata ziliokoa maisha yetu au kuwezesha matumizi yetu kwa kiwango bora.
Kuachilia kunaweza kuwa na maumivu, ni kama kuachana na rafiki wa zamani. Hatua ya Nne, Tano, Sita, na Saba hutusaidia kutambua na kubadilisha ujuzi huu wa zamani wa kuishi. Vifaa hivi vya kuishi havihitajiki tena katika Njia hii Mpya ya Maisha.
Katika Narcotics Anonymous tunapewa Sanduku la Vifaa vya Kiroho. Tunafanya Vifaa hivi viwe na ufanisi kwa kuvitumia katika Maisha yetu ya kila siku. Kanuni za Kiroho zilizomo katika Hatua na Mapokeo zinatufanya kuwa watu bora.
Pia zinawapa waraibu wengine Matumaini, kwamba nao pia wanaweza kupata Njia Mpya ya Kuishi. Tunagundua kwamba tunapozitegemea kasoro, tunajikuta katika maumivu na kuwaumiza wengine. Tunapozitegemea Kanuni za Kiroho maisha yetu na maisha ya wale walio karibu nasi yanapata manufaa.
Tunaweza kubeba Ujumbe wenye ufanisi, kwa sababu tunaishi. Kwa Msaada wa Nguvu yetu ya Juu, Wadhamini wetu na Jumuiya ya Narcotics Anonymous, tunaishi maisha safi na yenye tija. Hatupigani tena na hasira au unyogovu.
Tunajisalimisha kwa Mchakato na Maisha yetu ni Mapya. Tunaweza tu kuweka Zawadi hii ya Thamani, ikiwa tutaitoa.
Kwa
Tutachilia na Kumwacha Mungu afanye kile ambacho hatuwezi kufanya wenyewe.