Loading

Tafakari ya Kitabu cha Kijivu

29 Juni

Hii ni njia yetu ya ukuaji wa kiroho. Hii haitokani na kutamani, bali kutoka kwa vitendo na maombi.

Gray Book, pg. 49 (Step Seven, Lines 31-36)

Soma tafakari

Matamanio na ndoto zilikuwa baadhi ya mambo ambayo ugonjwa wa uraibu ulituibia kabla ya kutimizwa, au katika baadhi ya matukio, hata kabla ya kuendelezwa. Matumaini yetu yakawa matamanio, na matamanio yetu yakawa ndoto. Ugonjwa wa uraibu hata ulituondolea hayo, tukabaki na kukata tamaa na kutokuwa na uhakika.

Baada ya kufika katika Narcotics Anonymous tuliona Matumaini na ndoto zetu kwa wengine, lakini bado tulishindwa kuyaona katika Maisha yetu wenyewe. Tunapofanya Hatua, tulionekana kuamka na ukungu ukaondolewa. Miili na akili zetu hazikuwa tena zimejaa dawa za kulevya.

Wakati hamu ya kutumia ilipoondolewa katika Hatua ya Pili, tulianza kuhisi Matumaini. Tulifanya Hatua na Mungu na Wadhamini wetu.

Kitabu chetu cha Gray kinatuambia kwamba, "kwa uangalifu na urahisi tunajiondoa kutoka kwenye upweke wa uraibu hadi kwenye mkondo wa Ushirika wenye manufaa.' Tunaanza kuona kwamba chochote kinawezekana, hata ndoto zetu zilizopotea. Tukiandika Hatua yetu ya Nne tunaona tulipokosea, tunaona vikwazo vyetu, ambavyo katika hali nyingi vilikuwa sisi wenyewe.

Tunaanza kuachiliwa kutoka kwenye magereza yetu tuliyojitengenezea wenyewe. Tunapoandika Tathmini yetu ya Uaminifu ndoto zetu zilizopotea zinaanza kuonekana tena polepole, matamanio yetu na ndoto zetu yanakuwa Matumaini. Matumaini yetu yanakuwa Uhalisia tunapofanya kazi na Kuishi Kanuni za Kiroho za Hatua hizo. Tunashiriki Matumaini haya na wengine wanaposhuhudia yakidhihirika katika Maisha yetu.

Wakati Huu
✦   ✦   ✦

Tutakoma kutamani na kuanza kufanya kazi, ndoto zetu zilizopotea zinaweza kuwa Uhalisia tunapobaki katika Safari hii ya Urejesho.

Shiriki tafakari kwenye WhatsApp