Loading

Tafakari ya Kitabu cha Kijivu

4 Februari

Katika Hatua ya Kumi tunajitahidi kwa unyenyekevu wa kweli. Katika unyenyekevu huu tunaweza kuingiliana vizuri na wengine.

Gray Book, p. 56 (Step Ten, Lines 25-26)

Soma tafakari

Hatua ya Kumi inatufanya tuwe na Msingi wa Kiroho, hivyo tunaendelea kuchukua hesabu ya kibinafsi. Katika hesabu hii tunachukua hesabu ya mali zetu na madeni yetu, na tunakubali zote mbili. Kwa kutekeleza Kanuni za Narcotics Anonymous, hatuwezi kukanyaga vidole vya wenzetu. Kuchukua hesabu ya kila siku kunatuonyesha mahali tumekosea.

Tunafuata upungufu wetu kwa kufanya marekebisho. Hesabu yetu pia inaonyesha mahali tumekuwa sawa.

Kwa hivyo kwa sisi Kutekeleza Kanuni za Kiroho hatuwezi kutekeleza kasoro zetu. Kupitia utambuzi wetu na Kukubali kuwa binadamu na kuwa na kasoro kwa asili, tunaanza kukuza Uvumilivu na Ustahimilivu na sisi wenyewe. Wakati huo huo, tunakuza Uvumilivu na Ustahimilivu na wengine. Hatua zote na Desturi za Narcotics Anonymous zinahusiana na Kujisalimisha.

Kwa kiwango fulani hatua zote na desturi zinahusiana na kuchukua hesabu. Tunapitia kile kinachotufaa na kile kisichotufaa.

Tunatupa zana za zamani na kuchukua zana mpya. Uraibu huathiri kila eneo la Maisha yetu. Tunahitaji Kutekeleza Kanuni za Kiroho katika kila eneo la Maisha yetu, ili kuendelea katika Safari hii ya Kiroho.

Wakati Huu
✦   ✦   ✦

Tutaendelea katika Safari hii ya Kiroho kwa kuendelea na Mchakato wa Hesabu ulio katika Hatua na Desturi.

Shiriki tafakari kwenye WhatsApp